About

Swahilituts ni muunganiko wa maneno mawili yaani(Swahili + Tutorials(mafundisho)). Program hii ilianzishwa kwa malengo mahsusi ya kutoa Mafundisho(Tutorials) za jinsi ya kutumia softwares mbalimbali katika Computer kwa lugha ya kiswahili.

Kwa nini lugha ya kiswahili?
Tuliamua kutumia lugha ya kiswahili kwa sababu
  1. Kiswahili ni lugha yetu ya nyumbani.Hivyo tuna uelewa mkubwa wa matumizi yake tofauti na lugha nyingine za kigeni kama Kiingereza, Kiespaniola na nyinginezo.
  2. Katika tafiti zilizofanyika, imegundulika kwamba mwanafunzi au mtu yeyote anayejifunza somo fulani kwa kutumia lugha ya nyumbani anauwezo wa kuelewa somo hilo zaidi ya kuliko angetumia lugha za kigeni.Tunarudi palepale kwamba ni kwa sababu ana uelewa wa lugha husika tangu akiwa mtoto. Nchi nyingi zilizoendelea kiteknologia, mathalan China,Russia,U.S.A, Japan, Germany zinatumia lugha zao za kitaifa katika kufundishia. Hivyo tumeamua kutoa na sisi mafundisho hayo ka lugha ya kiswahili.
  3. Kwa kutoa Tutorials  kwa lugha ya kiswahili tunachangia kukua na kuenea kwa lugha yetu ndani na nje ya nchi pia.
  4. Pia kiswahili ni mojawapo kati ya lugha saba duniani zinazojulikana kama lugha za Kimataifa. Hivyo tunakila sababu ya kujivunia na kuitumia lugha yetu kufundishia.
  5.  
Tutakua tunatoa tutorials za vitu gani?
Ni vema kujua vitu ambavyo swahilituts tutavifundisha ili uweze kujua ni vitu gani tunavifundisha. Swahilituts tutakua tunafundisha vitu vifuatavyo:-
  
 1. Graphics Design
      Software ambazo tutazitumia ni:-
  • Adobe Photoshop
  • Adobe After Effects
  • Adobe Illustrator
  • Adobe Flash
  • Premier Pro
  • 3D MAX
  • CINEMA 4D
  • Cartoon Animator
 2. Presentation and Reports softwares
 3. Microsoft Office
  • Microsoft World
  • Microsoft Acces
  • Microsoft Excel
  • Microsoft Outlook
  • Microsoft Publisher
  • Microsoft PowerPoint
 4. Android app developments
 5. System developments
  •  Visual Basics(VB)
 6. Web development
  • PHP
  • JAVASCRIPT
  • HTML5
  • CSS

No comments:

Post a Comment